UBINGWA wa Ligi Kuu Bara msimu huu ni kama kaa la moto, kwani timu zinazokimbizana kileleni zile tatu kila moja ipo mawindoni ikilisaka taji ambalo lipo mikononi mwa Yanga inayopambana kulitetea.
Vita hiyo ya kusaka ubabe wa mashindano hayo imekuwa ikiibua mbinu na wakati mwingine kupanga ujanja wa ndani na nje ya uwanja, ambapo Simba, Yanga na hata Azam zote zinapambana pia kuweka mambo sawa.
Lakini, wakati Ligi Kuu Bara ikizidi kupamba moto raundi ya pili ya msimu, Kocha wa Simba Fadlu Davids ametaja dakika 270 ambazo kwa namna yoyote ile anapaswa kuzicheza au kuzitumia kwa akili kubwa sana kuupata ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Kimsimamo mpaka sasa Simba inashika nafasi ya pili katika ligi, ikiwa na alama 50 imebakiza mechi 11 kumaliza msimu, sita zikiwa za nyumbani na tano za ugenini.
Hesabu za Fadlu ambaye ni raia wa Afrika Kusini, msimu huu ni kuhakikisha anamalizia hesabu zake kwenye mechi tatu. Dhidi ya Azam, Yanga na Singida Black Stars ambazo ni sawa na dakika 270. Raundi ya kwanza alishazifunga Azam na Singida kwao, huku akifungwa na Yanga kwake.
Simba katika mechi tisa za nyumbani kwa maana ya zile ilizocheza Dar es Salaam, imeshinda michezo saba, kupoteza mmoja na sare moja. Imevuna pointi 22 Dar es Salaam, Yanga ina pointi 27 nyumbani ikifuatiwa na Azam 25 lakini wote wameizidi Simba michezo.
Timu hizo zinazokimbizana katika msimamo wa ligi,tatu zimecheza mechi 20, huku Simba pekee ikiwa imecheza mechi 19. Kwenye msimamo wa jumla, Yanga inaongoza kwa alama 52,Simba 50,Azam 43 na Singida Black Stars ikiwa nazo 37.
Akizungumza na Mwanaspoti, Fadlu alisema amewaambia wachezaji wake ili mbio zao za kwenda kuufuata ubingwa ziwe na urahisi, basi mechi hizo tatu kubwa lazima wakaziamue kwa pointi tatu na ikiwezekana goli za kutosha.
“Safari yetu kuufuata ubingwa itaanzia kwa Azam, ambao licha ya kuwafunga kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza tunatakiwa kuwafunga tena kwenye unaofuata ili waweze kuendelea kujiweka salama.
“Tangu wapoteze dhidi ya Yanga hatujafungwa tena hii inaonyesha hizi mechi zingine sio shida kubwa kwetu ni kuongeza umakini na kutumia nafasi vizuri.”
Simba itaikaribisha Azam Jumatatu ya Februari 24 katika Uwanja wa KMC Complex, Majira ya Saa10:00 Jioni.
Kutokana na rekodi zilizopita Fadlu anakazi ya kufanya kwa Yanga ambayo imekuwa ikiisumbua Simba tangu msimu uliopita, ukilinganisha na Azam na Singida ambazo amekuwa akizifunga.
Rekodi za timu hizi katika misimu mitatu iliyopita,