Scholz Hatarini Kuangushwa Ukansela Ujerumani – Global Publishers



Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz, amekalia kuti kavu katika uchaguzi unaoendelea ambapo matokeo ya awali yanaonesha kuwa mpinzani wake, Friedrich Merz kutoka Chama cha Christian Democratic Union (CDU), anaongoza kwenye kura za awali.

Endapo matokeo yataendelea kubaki hivyo, Merz ataingia kwenye rekodi ya kuwa kansela mwenye umri mkubwa zaidi akiwa na miaka 69, tangu Konrad Adenauer aliposhika wadhifa huo mwaka 1949 akiwa na umri wa miaka 73.

Kama ilivyo kwa Scholz, Merz naye ni mwanasheria, na kwa takribani miaka 12 alikuwa hajishughulishi kabisa na siasa mpaka mwaka 2021 aliporejea, ambapo alianza kutajwa kuwa mpinzani mkubwa wa Scholz aliyeingia madarakani kumrithi Angela Merkel.


Related Posts