WANANCHI WA RUVUMA WAMETAKIWA KUTUNZA MAKUMBUSHO YA VITA VYA MAJIMAJI

 NA BELINDA JOSEPH, RUVUMA

Wananchi Mkoani Ruvuma wametakiwa kutunza na kuenzi makumbusho ya  vita vya Majimaji kwa lengo la kutambua juhudi zilizofanywa na mashujaa hao katika kupigania haki zao, kwani kuanzishwa kwa Kumbukizi hizo kunalenga kuendeleza urithi, umoja pamoja na amani kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Peresi Magiri, alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwenye hafla ya uzinduzi wa Tamasha la Kumbukizi ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji Februari 23 Wilayani Songea Mkoani Ruvuma, amesema wananchi wanawajibu wakuendelea kuwakumbuka mashujaa 67 waliopigana vita wakitetea haki zao Februari 27.

Kufuatia Uwepo wa Tamasha la Kumbukizi hizo ameeleza kuwa wamejikita katika kuendeleza sekta ya utalii, kwa kuinua uchumi wa Watanzania huku akiahidi kuendeleza ushirikiano na wizara ya Maliasili na utalii, pamoja na wizara ya utamaduni katika kuendeleza mazuri yote yaliyoanzishwa na viongozi waliotangulia, kwani maendeleo yanahitaji amani na ushirikishwaji wa dhati na kwa wakati mwafaka.

Akizungumza Inkosi wa Mankosi Emmanuel Zulu Gama, amewataka Watanzania kuendelea kuwakumbuka Mashujaa walionyongwa,  huku wakiendelea kuziombea familia zilizoathirika zipate haki zao kwani mpaka hivi Sasa bado zinalia kwa kuondokewa na ndugu zao kwa namna Ile kwa kuondoka na viwiliwili ikiwa mchakato wa kurejesha amesema bado unaendelea.

Tamasha la kumbukizi ya Vita vya Majimaji limezinduliwa rasmi hii leo Februari 23 na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma DC Peresi Magiri na kufuatiwa na Mashindano ya ngoma, Vyakula na dawa za asili, Mdahalo Utakaofanyika Namtumbo, siku ya Wangoni Maposeni Peramiho ambapo linatarajiwa kuhitimishwa Februari 27 na mgeni rasmi Jenerali Jacobo Mkunda, chini ya Kauli mbiu isemayo “Makumbusho ya Majimaji na mali kale zetu kwa maendeleo ya Utalii na Uchumi”, hivyo ni jukumu la kila Mmoja kushiriki kumbukizi hizi Muhimu kwa lengo la kuwaenzi washujaa wa Taifa hili.

Related Posts