Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimeandaa Kongamano maalum kwa ajili ya kumuenzi aliyekuwa Mkuu wake wa Kwanza chuo hicho, Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi.
Kongamano hilo la siku tatu litakalofanyika katika Kituo cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu, Kampasi ya Mloganzila, litatanguliwa na matukio mbalimbali ambapo Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi atakuwa mgeni rasmi siku ya kilele chake, Februari 28.2025
Kongamano hilo linaangazia mchango wa Hayati Ali Hassan Mwinyi katika maendeleo ya elimu, afya, na ustawi wa jamii, na litajumuisha shughuli mbalimbali muhimu, ikiwemo Uzinduzi wa Mfuko wa Maendeleo wa Ali Hassan Mwinyi, uzinduzi wa Kongamano la Kila Mwaka la Ali Hassan Mwinyi, Kurejesha Vazi Rasmi la Mkuu wa Kwanza wa Chuo kwa Familia, Maonyesho ya Afya na Elimu, Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo cha Tiba na Kambi Maalum ya Huduma za Afya, 26-27 Februari 2025