MAAFISA WA TUME YA UCHAGUZI WAFANYA ZIARA KATIKA VITUO VYA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA ZANZIBAR.

 

 

Na Rahma Khamis Maelezo 24/2/2025

Zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura awamu ya pili limekwenda vizuri katika Wilaya ya Kaskazi A’ ambapo wananchi walio wengi wamejitokeza kujiandikisha katika daftari hilo ili kupata haki yao ya msingi .

Akizungumza mzra baada ya kutembelea vituo vya uandikishaji wa daftari hilo Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe, Jaji Aziza Idd Suwed amesema kuwa zoezi lilifanyika kwa Amani na utuli na kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa katika daftari alipata haki yake ufanikiwa kuwaingiza katika mfumo .

“Tunashukuru zoezi limekwenda vizuri na hadi sasa hakuna matatizo yoyote ambayo yamejitokeza isipokua changamoto ndogondogo za wananchi wenyewe kutokana na vidole lakini tumeweza kuzitatua tunashkuru,”alisema Makamu kukesho Febuary 25.

Amesema Tume inaendelea na zoezi la uwandikishaji wa daftari hilo ambapo kesho wanatarajia kuanza Wilaya ya Kasazini B’ ili wananchi wa huko wapate haki yao ya msingi

Aidha amefahamisha kuwa zoezi la kuvitembelea vituo hivyo limeanza Jumamosi na kuendelea hadi kufikia leo Febuary 24 ambapo wamefanikiwa kutembelea vituo13 kwa zoni ya Mkwajuni.

Hata hivyo Jaji Aziza amewashajiisha wananchi w Wilaya nyengine kujitokeza na kujiandaa kujiiandikisha katika daftari hilo.

Nao Wakuu wa Vituo vya kujiandikisha akiwemo Sabra Mhamed Khamis kutoka Kibeni na Miza Juma Haji kutoka Moga wamefahamisha kuwa tangu kuanza zoezi hilo hakuna tatizo lolote lililojitokeza kwai wamekwenda vizuri hadi kukamilika kwake.

Zoezi la uandikshaji wa daftari la wapiga kura linaendelea kesho katika Wilaya ya Kaskazini B’ambapo kwa leo limekamilika katika Wilaya ya Kaskazini A’katika vituo mbaimbali iikiwemo Kivunge,Kibeni,Chaanikubwa,Chaanimchezashauri,Chaanimasingini,Kikobweni,Bandamaji na GambaMsimamizi mkuu wa Kituo cha Uandikishaji Wapiga Kura Shehia ya Kinyasini Kalathumi Kondo Makame akizungumza kuhusiana na Zoezi la Uandikishaji linavyoendelea katika Kituo hicho wakati wa Ziara Maalum ya Maafisa wa Tume ya Uchaguzi kutembelea Maeneo ya Uandikishaji na kusikiliza Changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia Suluhisho katika Mkoa wa Kaskazini A Unguja.Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Aziza Iddi Suwed (kushoto) akimsikiliza Naibu Sheha wa Shehia ya Banda Maji Fadhili Mshamba Juma akizungumzia kuhusiana na Uandikishwaji wapiga Kura katika Shehia hio katika Ziara Maalum ya Maafisa wa Tume ya Uchaguzi kutembelea Maeneo ya Uandikishaji na kusikiliza Changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia Suluhisho katika Mkoa wa Kaskazini A Unguja.Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Aziza Iddi Suwed (kushoto) akimsikiliza Mmoja kati ya Mawakala wa Vyama akizungumzia kuhusiana na Zoezi la Uandikishwaji wapiga Kura linavyoendelea katika Shehia ya BandaMaji wakati wa Ziara Maalum ya Maafisa wa Tume ya Uchaguzi kutembelea Maeneo ya Uandikishaji na kusikiliza Changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia Suluhisho katika Mkoa wa Kaskazini A Unguja.Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Aziza Iddi Suwed akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wasimamizi wa Uandikishaji Wapiga kura Shehia ya Masingini wakati wa Ziara Maalum ya Maafisa wa Tume ya Uchaguzi kutembelea Maeneo ya Uandikishaji na kusikiliza Changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia Suluhisho katika Mkoa wa Kaskazini A Unguja.Muandikishaji Wapiga Kura katika Shehia ya Kikobweni akimsaidia Mwananchi aliefika kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura wakati wa Ziara Maalum ya Maafisa wa Tume ya Uchaguzi kutembelea Maeneo ya Uandikishaji na kusikiliza Changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia Suluhisho katika Mkoa wa Kaskazini A Unguja.Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Aziza Iddi Suwed akiwa pamoja na Maafisa wa Tume ya Uchaguzi katika Ziara Maalum ya Maafisa hao kutembelea Maeneo ya Uandikishaji Wapiga Kura na kusikiliza Changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia Suluhisho katika Mkoa wa Kaskazini A Unguja.Muandikishaji Wapiga Kura katika Shehia ya Kinyasini akimsaidia Mwananchi aliefika kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura wakati wa Ziara Maalum ya Maafisa wa Tume ya Uchaguzi kutembelea Maeneo ya Uandikishaji na kusikiliza Changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia Suluhisho katika Mkoa wa Kaskazini A Unguja.

Related Posts