MSHINDI WA KITILA JIMBO CUP KUPATA BAJAJ

 

Michuano ya soka inayofahamika kama Kitila Jimbo Cup iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo inatarajiwa kuhitimishwa February 28 mwaka huu.

Fainali za michuano hiyo zitafanyika katika Uwanja wa Kinesi kwa kuzikutanisha timu za Wima kutoka Kata ya Mburahati na Baruti kutoka Kata ya Kimara.

Nafasi ya Tatu inawaniwa na Timu za Kimara Combine kutoka Kata ya Kimara na Lamasia kutoka Kata ya Makurumla ambazo zitaanza kwa mechi ya utangulizi kabla ya mechi ya fainali.

Mshindi wa jumla katika michuano hiyo iliyoandaliwa na Mbunge wa Ubungo Prof. Kitila Mkumbo atapatiwa Bajaji mpya, mshindi wa Pili atapatiwa Pikipiki na mshindi wa Tatu atapatiwa Sh. Milioni 1.

Michuano hiyo ambayo imehusisha timu 16 kutoka kila Kata timu mbili, nusu fainali yake imepigwa February 22 mwaka huu ikitanguliwa na Jogging iliyohusisha watu mbalimbali na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Lazaro Twange.

Akizungumza baada ya kuhitimisha jogging hiyo Mkuu wa Wilaya huyo amesema michezo ni Afya na inaimarisha umoja na mshikamano na kumpongeza Prof. Kitila Mkumbo kwa kuanzisha Kitila Jimbo Cup ambayo imekuwa na hamasa kubwa.

Mwisho

Related Posts