Dkt. Pallangyo Awasihi Wahitimu wa AKU Kuwa Wabunifu na Wenye Maono


CHUO Kikuu cha Aga Khan (AKU) kimefanya mahafali 20 kwa mwaka wa masomo 2024/2025, ambapo wahitimu 71 kutoka fani mbalimbali wamepokea shahada zao. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 24, 2025 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa chuo, wanazuoni, wanafamilia wa wahitimu, pamoja na wageni mashuhuri.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan, Dkt. Eunice Pallangyo, amesisitiza dhamira ya chuo hicho katika kutoa elimu bora tangu kilipoanzishwa mwaka 2002. Alieleza kuwa AKU inawapokea walimu waliopo shuleni wanaokuja kujiendeleza kimasomo ya shahada ya pili, wahitimu kutoka Shule ya Uuguzi na Ukunga, pamoja na madaktari wanaoendelea na masomo yao chuoni hapo.
Dkt. Pallangyo amewataka wahitimu kufanya kazi kwa ubora, ubunifu, na kuwa mstari wa mbele kuleta mabadiliko katika jamii zao. “Tunahitaji watu wanaotumia ujuzi wao kwa manufaa ya jamii, siyo walalamikaji. Kuwa mbunifu na kujiamini ni nguzo muhimu za mafanikio,” amesisitiza.
Aidha, amebainisha kuwa chuo kinaendelea na programu mbalimbali, ikiwemo shahada ya miaka miwili ya Uuguzi, inayolenga kusaidia sekta ya afya nchini.


Malkia Zahra Aga Khan amesema elimu ni nguzo muhimu ambayo Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, uwamekuwa wakiyapa kipaumbele kwa kuwa ndio msingi wa kuboresha maisha ya wananchi.

Malkia huyo amesema baba yake alianzisha vyuo vikuu viwili ambavyo ni Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU) na Chuo kikuu cha Asia ya Kati (UCA), kwa lengo la kuimarisha mfumo wa elimu.

Katika nahafali hayo ya chuo hicho kilitoa heshima kwa mwanzilishi na mkuu wa kwanza wa kwanza wa chuo, hayati Aga Khan wa nne na kumkaribisha mrithi wake mfalme Rahim Aga Khan wa tano.

 Kufanyika kwa malhafali hayo, Malkia Zahra amesema ilikuwa ni fahari kwa baba yake kuona kila mtu amehitimu elimu yake ndani ya chuo hicho, huku akidokeza wahitimu wa mwaka huu ndio wa mwisho kusoma chini ya busara ya baba yake. “Naishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutupa imani kwa muda mrefu hasa katika utekelezaji wa maono ya taasisi yetu ya kufungua fursa sekta ya elimu na kuboresha sekta ya afya,”amesema.

Mahafali haya yalijawa na furaha, huku familia na marafiki wakisherehekea mafanikio ya wahitimu. Chuo Kikuu cha Aga Khan kimeendelea kuwa kinara wa elimu bora, kikiwahamasisha wanafunzi wake kuwa viongozi wa mabadiliko na wabunifu katika taaluma zao.
Mhitimu wa shahada ya umahiri katika Uandishi wa Habari, Absoulum Kibanda, amesema kuwa fursa aliyopata chuoni imemwandaa kushiriki kikamilifu katika kuwaandaa vijana kukabiliana na changamoto za kimtandao.
“Sisi kama wanataaluma wa uandishi wa habari tunalo jukumu la kuwa wabunifu ili kufanya Citizens Journalism iwe na vigezo vya udhibiti, hivyo kuboresha na kukuza taaluma kwa weledi,” alisema Kibanda.
Kwa upande mwingine, wahitimu wameeleza kuwa masomo waliyopata yatawawezesha kuboresha huduma katika sekta zao kwa ubunifu na ufanisi mkubwa.

Related Posts