Sababu wanafunzi kusahau wanayofunza darasani

Ajabu ya kumbukumbuku ni kuwa tunasahau tunayotaka kukumbuka na tunakumbuka tunayotaka kusahau.

Kusahau ni sehemu ya maumbile ya binadamu; inabidi mtu asahau ili taarifa zingine zihifadhike. 

Usahaulifu ninaozungumzia ni ule wa mtu kutaka kukumbuka halafu anasahau na hasa wanafunzi wanapokuwa wanajiandaa na mitihani au wakiwa ndani ya chumba cha mitihani. Sababu zinazowafanya wanafunzi wasahau ni hizi:

Mosi, kutopitia somo baada ya kufundishwa. Wataalamu wa mambo ya usomaji, wanasema mwanafunzi anapofundishwa somo, anapaswa kulipitia somo hilo hata kama kama hana ratiba ya kulisoma soma hilo;lengo ni kuhifadhi uelewa wake kwani asipofanya hivyo atapoteza uelewa wa somo kwa asilimia 58.

Pili, kusoma vitu vingi kwa wakati mmoja.Hali hii inasababisha kuwapo kwa ushindani wa taarifa za zamani(retroactive interference) na taarifa mpya (pro active interference) jambo linalomfanya mwanafunzi kusahau baadhi ya vitu.

Kwa mfano, anaingia kwenye chumba cha mtihani kila akijaribu kukumbuka taarifa inakuwa kama inakuja ila inaishia nn njiani. Hii ni kwa sababu ya kusoma vitu vingi kwa wakati mmoja.Ajabu akitoka tu kwenye chumba cha mtihani anakumbuka!

Tatu,kuchoka kwa akili. Hakuna ambacho kinaweza kueleweka na kuhifadhika pindi akili inapochoka. Unapohisi akili imechoka fanya yafuatayo;hesabu moja hadi 20 kwa kinyumenyume, yaani 20,19,18,17,16,15,14,13,12,11,10,9,8,7,6,5,4,3,2,1.Fanya hivi mara tatu kwa spidi ya kawaida ila ukiona unapatia ni kipimo kuwa akili haijachoka ila ukiona unakosea, unahitaji kupumzika kwani ni ishara akili imechoka.

Nne,maandalizi mabaya unakapokaribia mtihani.Wanafunzi  wana tabia ya kusoma sana wanapokaribia msimu au wanapokuwa ndani ya msimu wa mitihani na kujikuta wanasoma juujuu yaliyomo kwenye daftari au vitabu na hivyo kujikuta wanaegesha vitu badala ya kuelewa kwa kina.

Wapo wanaopenda kusoma masomo fulani tu na hivyo kuwekeza nguvu nyingi zaidi katika masomo hayo, bila ya kujua kuwa ufaulu unategemea masomo yote. Mwanafunzi anayesoma masomo fulani tu ni rahisi sana kwake kufanya vibaya kwani atawekeza nguvu zake katika somo fulani a kuacha masomo mengine,.

Jambo hili  litasababisha uelewa hafifu na kusahau yale aliyofunzwa kwa kuhisi somo hilo siyo muhimu sana katika ufaulu wake au maisha yake.

Tano, kutokuwa darasani kifikra kama anavyosema mwanasaikolojia, Daniel  Schacter kwenye kitabu chake cha “Seven Sins of Memory.

Mwanafunzi anaweza kuhama na kuwaza vitu vingine vingi ndani ya kipindi na hivyo kumfanya achukue kidogo sana yale yaliyofundishwa na mwalimu na hivyo kumfanya awe na uelewa hafifu na hata kusahau hicho kidogo alichokielewa.

Ndiyo maana ni muhimu kwa mwalimu kutumia njia shirikishi, ili kuwafanya wanafunzi wa aina hii kuwa darasani kiakili na hatimaye kuelewa somo.

Related Posts