TCAA YAKABIDHI SETI YA JEZI KWA TIMU YA MIGUU YA BARA FC

 

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeidhamini timu ya mpira ya chini ya miaka ishirini (U-20) ya Bara FC seti mbili ya jezi wakiwa wanaelekea katika michuano ya Ligi ya Kimkoa yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Akikabidhi jezi hizo Februari 25, 2025, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Daniel Malanga amesema, “Lengo la kurudisha kwa Jamii ni kushirikiana pamoja na wadau mbalimbali kwa kuchangia maendeleo yao na ya taifa kiujumla”.

Vilevile Bw. Malanga aliwatakia kila la kheri katika michuano hiyo ya Ligi ya Mkoa na kuwaasa kuendelea kutafuta wadhamini wengine ili wachezaji waweze kufanya kazi nzuri Zaidi na kuwaasa wachezaji kuweka juhudi ili waweze kupanda madaraja la juu zaidi na hatimaye ligi kuu.

Naye Mwenyekiti wa Timu ya Bara FC, Bw. Khatib Kikaji aliishukuru Mamlaka kwa udhamini huo wa jezi walioupata na kuomba ushirikiano zaidi ilI waweze kutimiza malengo yao.

Bara FC imeweza kushiriki mashindano hayo baada ya kuibuka mshindi wa pili katika Mkoa wa Dar es Salaam, na wataweka kambi mjini Mtwara ili kujiandaa na mashindano hayo ambapo imepangwa katika kundi A.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Daniel Malanga (wa pili kulia) akikabidhi jezi kwa Mwenyekiti wa Timu ya Bara FC, Bw. Khatib Kikaji(wa pili kushoto) kwa timu ya mpira ya chini ya miaka ishirini (U-20) ya Bara FC
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Daniel Malanga (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Timu ya Bara FC, Bw. Khatib Kikaji(wa pili kushoto) wakionesha jezi za timu ya mpira ya chini ya miaka ishirini (U-20) ya Bara FC zilizodhaminiwa na Mamlaka hiyo

Related Posts