Samia ateua mrithi wa Mafuru

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investiment (WHi), Dk Fred Msemwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango.

Taarifa ya kuteuliwa kwake imetolewa leo, Februari 27, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Sharifa Nyanga.

Dk Msemwa ameteuliwa kushika nafasi hiyo iliyokuwa wazi kwa siku 110 kufuatia kifo cha aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Lawrence Mafuru kilichotokea Novemba 9, 2024

Mafuru alifariki dunia akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Apollo nchini India.

Mafuru aliyekuwa mtaalamu wa fedha na uchumi maarufu hapa nchini, amehudumu katika taasisi kubwa tofauti kwa miongo miwili.

Amewahi kuwa Msajili wa Hazina na Ofisa mtendaji mkuu wa Benki ya

Pia amewahi kuwa Naibu Katibu wa

Wizara ya Fedha, Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki nchini (TBA) na mwanzilishi wa mwenza wa kampuni ya ushauri wa masuala ya fedha ya Bankable.

Dk Msemwa anashika nafasi hii akiwa ni mbobezi katika kaguzi za hesabu, mtaalamu wa biashara na amewahi kuandika kitabu kiitwacho ‘Usimamizi wa Biashara na Fedha’.

Pia anatambulika kwa mchango wake katika kuendeleza upatikanaji wa nyumba za gharama nafuu, uongozi wa bodi za kampuni mbalimbali, uwezeshaji wa vijana na utetezi wa biashara ndogondogo nchini Tanzania.

Wengine walioteuliwa ni Profesa Philipo Lonati Sanga kuwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kabla ya uteuzi huu, Profesa Sanga alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

Profesa Sanga anachukua nafasi ya Profesa Michael Ngumbi ambaye amemaliza muda wake.

Pia Balozi Susan Kaganda amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

Kaganda anapangiwa kitu cha kazi ikiwa ni zaidi ya miezi miwili tangu apewe hadhi hiyo Desemba 8, mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu uapisho wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Related Posts