Ikiwa leo hii ni Alhamisi wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet wameendelea na kurejesha kwenye jamii ambapo leo hii waliamua kuwafikiwa wakazi wa Mbezi Juu kwaajili ya zoezi zima la upandaji miti.
Zoezi hili limefanyika kwa ushirikiano mkubwa na wafanyakazi wa Meridianbet, wananchi wa hapo Mbezi ambao waliwapokea Meridianbet kwa furaha kubwa zaidi wakiongozwa na kiongozi wa eneo hilo.
Meridianbet, kupitia mpango huu, inaendelea kujitolea kwa jamii kwa kuimarisha uhusiano wake na wananchi na kuchangia katika maendeleo endelevu ya mazingira na jamii kwa ujumla. Kampuni hii inaendelea kuwa kielelezo cha uwajibikaji katika jamii na kuhamasisha ushirikiano katika uboreshaji wa mazingira.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mwakilishi wa Meridianbet alisema: “Sisi kama Meridianbet tunaamini katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii tunayohudumia. Kupitia mpango huu wa upandaji miti, tunalenga kuboresha mazingira na kuhakikisha kizazi cha sasa na kijacho kinapata faida za miti, ikiwa ni pamoja na hewa safi na ardhi yenye rutuba. Tunawashukuru wote walioungana nasi katika kampeni hii muhimu.”
Meridianbet imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza miradi ya kijamii (CSR) kwa kuwekeza katika mazingira, elimu, afya, na maendeleo ya jamii kwa ujumla. Kampuni inaendelea kujitolea kwa dhati kuboresha maisha ya Watanzania kupitia programu mbalimbali za kijamii.