Mzee wa miaka 62 aliyezikwa akiwa hai kwa siku nne aokolewa na polisi

Katika tukio la kushangaza huko Moldova, polisi walimuokoa mwanamume mmoja ambaye alikuwa amezikwa akiwa hai kwa siku nne.

Maafisa walikuwa wakichunguza kifo cha mwanamke mwingine mwenye umri wa miaka 74, aliyepatikana nyumbani kwake na ndipo  waliposikia vilio vya kuomba msaada karibu na walipochimba, waligundua mlango wa chumba cha chini cha ardhi ambapo mzee wa miaka 62 alikuwa amefungwa na kijana ambaye baadae alinaswa na polisi.

Vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti kuwa tukio hilo lilitokea Mei 13 na mwanamume aliyeokolewa alikuwa  na jeraha la shingo.

Polisi baadaye walimkamata kijana wa miaka 18 kutoka nyumbani kwake huko Ustia, kaskazini magharibi mwa Moldova, aliyehusishwa na kesi hiyo, kama ilivyoripotiwa na Need To Know.

Alipoulizwa, kijana huyo alitoa majibu ya kutatanisha, hali iliyowafanya polisi kupekua nyumbani kwake ili kupata ushahidi zaidi.

 

Related Posts