Katibu Mkuu, Wizara ya
Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, kilichofanyika
jijini Dodoma, ambapo walijadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya
nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Dkt. Mwamba, aliishukuru Serikali ya Japan kwa kuendelea kuwa wadau muhimu wa maendeleo ya nchi.
Kikao
hicho pia kilihudhuriwa na Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Dkt.
Johnson Nyella, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya
Fedha, Bw. Melckezedeki Mbise, Mchumi kutoka Wizara ya Fedha Bw. Edson
Vedasto na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Bw. Robert Bendera.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akisalimiana na Balozi wa Japan
nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami alipofika Ofisi za Wizara ya Fedha,
Dodoma kwa ajili ya mazungumzo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati wa kikao na Balozi
wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, aliyefika katika Ofisi
za Hazina-Treasury Square, Jijini Dodoma, kujitambulisha na kujadili
masuala mbalimbali ya ushirikiano Kati ya pande hizo mbili..
Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, baada ya kufika ofisini
kwake, Jijini Dodoma, kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
Kikao kikiendelea kati ya
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa
Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, ambaye alifika ofisini kwake
kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
pande hizo mbili.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa Japan nchini Tanzania,
Mhe. Yoichi Mikami wakiongoza ujumbe wa Tanzania na Japan katika picha
ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao kati yao, kilichofanyika jijini
Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akiteta jambo na
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw.
Melckzedek Mbise, wakati wa kikao kati yake Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, ambaye alifika ofisini kwake Jijini
Dodoma, kwa ajili ya kujitambulisha..
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano WF, Dodoma)