Serikali ya Ujerumani imetakiwa kuimarisha mipango yake ya ulinzi wa mazingira kutokana na hatua zilizoko hadi sasa kuonesha ufanisi kidogo wa kufanikisha malengo ya nchi ya mazingira.
Soma: Ujerumani: Itashirikiana na Tanzania katika utunzaji wa mazingira.
Uamuzi huo umetolewa na mahakama ya juu ya Berlin-Brandenburg, ambayo imeunga mkono kesi mbili zilizowasilishwa na shirika la ulinzi wa mazingira la Ujerumani Deutsche Umwelthilfe.
Uamuzi huo ulisema hatua za serikali ya shirikisho katika hali yake ya sasa hazikidhi mahitaji ya kisheria. Serikali ya shirikisho inaweza kukata rufaa katika mahakama ya utawala ya shirikisho na hivyo kuahirisha hukumu.
Shirika hilo limewahi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya sera ya serikali ya Ujerumani kuhusu mazingira na kushinda Novemba 2023.
Ujerumani Chama cha Kijani chaadhimisha miaka 40
Wakati huo, Mahakama ya Juu ya Utawala ya Berlin-Brandenburg iliamua kuwa serikali lazima ianzishe mpango wa dharura wa mazingira katika sekta ya uchukuzi na majengo. Rufaa dhidi ya hukumu hii kwa sasa inasikilizwa na Mahakama ya utawala ya shirikisho.
Hoja za kisheria za shirika hilo zilizingatia malengo yaliyowekwa katika sheria ya ulinzi mazingira ya Ujerumani, ambayo inataka kupunguzwa kwa uzalishaji wa gesi chafu katika kipindi cha 2024 hadi 2030. Aidha, sheria inaweka lengo la kupunguza uzalishaji wote huu kwa angalau asilimia 65 ifikapo mwaka 2030 ikilinganishwa na 1990. Hadi kufikia 2023 Ujerumani iliweza kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 46.
Mpango wa ulinzi wa mazingira unachukuliwa kuwa aina ya mpango wa jumla wa serikali ya shirikisho ili kufikia malengo haya. Unajumuisha hatua nyingi katika sekta za usafirishaji, nishati, majengo, na kilimo.