ILI kurahisisha upatikanaji wa gesi ya kupikia kwa gharama nafuu kwa Watanzania, Kampuni ya Total Energies Tanzania imewekeza kiasi cha dola za Marekani milioni saba (Sh 17 bilioni) katika kusambaza nishati hiyo safi ya kupikia kwenye maeneo mbalimbali ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Hayo yamebainishwa leo Ijumaa na Mkurugenzi wa Sheria, Uhusiano na Utawala kutoka Total Ernegies, Getrude Mpangile wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei 2024 kuhusu kampuni hiyo ilivyojipanga kuendelea uungaji mkono matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Amesema uongozi wa kampuni hiyo umedhamiria ifikapo mwaka 2030 zaidi ya watu milioni 100 kutoka India na nchi za Afrika, wanatumia nishati safi ya kupikia.
“Siku chache zilizopita tulizindua gesi mpya ya kupikia kwa gharama nafuu, tumejidhatiti kuhakikisha Watanzania wanapata nishati kwa gharama nafuu ndio maana katika mpango wetu tumedhamiria kwa kadiri ya mahitaji yao, tutawekeza katika namna rahisi na kuwapatia elimu ya matumizi ya nishati hiyo.
“Pia tutashirikiana na wadau walio tayari na wabunifu wakubwa na wadogo. Kwa mfano wiki mbili zilizopita tulizindua shindano kwa wajasiriamali na wabunifu wadogo ambao wanajihusisha na nishati safi ya kupikia tuliloita ‘Total energies Startup challenge’.
“Shindano linaendelea, tunaendelea kupokea maombi ya washiriki hadi 18 Juni mwaka huu hivyo nitoe wito kwa vijana kushiriki hasa shindano hili kipengele cha nishati safi,” amesema.