WATUMISHI WANAWAKE TCAA WAUNGANA NA WANAWAKE WENGINE KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, watumishi wanawake wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wameshiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa mkoani Arusha Machi 08, 2025, Mgeni Rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mhe.Rais Samia amepongeza jitihada zilizofanywa katika kuweka uwiano katika Nyanja zote kwenye jamii ya kitanzania.

“Kupitia marekebisho ya sera, sheria na jitihada mbalimbali tunazozichukua za kukuza uchumi, tumeweza kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo hili la kutokuwa sawa baina ya wanawake na wanaume.” amesema Rais Samia Suluhu.

TCAA imeshiriki katika ngazi ya kitaifa na kimkoa jijini Dar es Salaam ambapo watumishi wanawake wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) walioko jijini Dar es salaam wameshiriki maandamano kama sehemu ya maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders, Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Wanawake na Wasichana 2025:Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji.”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wananchi kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha tarehe 08 Machi, 2025. 

Watumishi wanawake wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakiwa katika picha ya pamoja katika Uwanja wa kumbukumbu ya Sheihk Amri Abeid jijini Arusha ambapo maadhimisho haya yanafanyika Kitaifa 

Related Posts