Ceasiaa Queens yalia na ratiba WPL

KOCHA wa Ceasiaa, Ezekiel Chobanka amesema mvurugano wa ratiba umeathiri kiasi kikubwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Mlandizi Queens.

Awali, mechi hiyo ilipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa TFF Kigamboni, Machi 12 lakini imesogezwa siku nne mbele huku sababu za kufanya hivyo zikiwa hazijulikani.

Akizungumza na Mwanaspoti, Chobanka alisema kama timu wanapambana kupata mechi angalau moja ya kirafiki ili kurejesha ufiti wa wachezaji.

“Kwa sisi ambao tuko mikoani hasa Iringa hakuna timu nyingine zinazoshiriki Ligi, tumekaa zaidi ya mwezi hamna mechi, napambana kuja mapema Dar es Salaam kupata mechi za kirafiki,” alisema Chobanka.

“Kuna haja TFF kuangalia namna nzuri ya kuweka mpangilio wa ratiba ili kusaidia na timu za mikoani ambazo zinatumia gharama kubwa za usafiri kufika Dar.”

Hii ni mara ya pili timu hizo zinakutana msimu huu, awali Ceasiaa ilishinda mabao 5-0.

Related Posts