TANZANIA KUWA MWENYEJI KILELE CHA SHINDANO LA KWANZA LA VIJANA AFRIKA KWENYE MASUALA YA AKILI MNEMBE NA ROBOTI.

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Tanzania kuwa mwenyeji wa kilele cha shindano la kwanza la vijana la afrika kwenye masuala ya akili mnembe na roboti(The african Youth in Artificial Intelligence and Robotics Competition).

Hayo ameyaeleza Jijini Dodoma leo na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdula alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa shindano hilo litafanyika Kuanzia tarehe 13-17 oktoba mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Katibu huyo amewataka watanzania kushiriki kwa wingi kwenye shindano la maadhimisho ya kilele cha mashindano ya bunifu za Akili Mnemba ili kudhibitisha utambulisho wa uwezo wa watanzania katika ramani ya wabunifu wa Akili Mnemba na Robotics Barani Afrika na Duniani kote.

Aidha amesema kuwa Katika kutekeleza Mkakati huo,nchi wanachama wanapaswa kuhamasisha
ubunifu wa vijana kwenye masuala ya Teknolojia zinazoibukia ikiwemo
masuala ya akili Mnemba.

“Serikali kwa kushirikiana na Wadau wengine, tutatoa ushirikiano wa kutosha
kuhakikisha kuwa maadhimisho haya yanafanikiwa na kuwa mfano kwa nchi
wanachama wa Umoja wa Afrika na Duniani kwa Ujumla,”amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo DKt Nkundwe Mwasanga, amesema kuwa Mwaka 2017, Tanzania pia ilianzisha kongamano la wataalam wa TEHAMA,mkutano huu ulianza kwa udogo ingawa sasa una sura ya kimataifa.

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imepewa jukumu la
kusimamia ukuaji na uendelezaji wa Sekta ya TEHAMA,Usimamizi huo
unaendana na uanzishwaji wa Sera, Sheria, miongozo pamoja na mikakati
mbali mbali inayohusu masuala na mabadiliko ya ukuaji wa TEHAMA
itakayowezesha matumizi salama na yenye manufaa ya Teknolojia
zinazoibukia (Kama Akili mnemba, robotics na kadhalika.







Related Posts