Aliyetaka Kujitoa Mhanga Ikulu Apigwa Risasi – Global Publishers



Ikulu ya White House, Marekani

Mtu mwenye silaha amejeruhiwa kwa kupigwa risasi na maafisa wa Secret Service nje ya Ikulu ya White House, Marekani, tukio lililotokea leo Machi 9, 2025.

Inaelezwa kuwa wakati wa tukio hilo, Rais wa Marekani, Donald Trump, hakuwepo katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa Anthony Guglielmi, Mkuu wa Secret Service, maafisa walipokea taarifa kuhusu mtu aliyekuwa na nia ya kujitoa mhanga, akisafiri kuelekea Washington D.C. kutoka Indiana.

Mtu huyo alionekana akikaribia White House, na maafisa walipomkaribia, alianza kutoa silaha na kuwatishia. Maafisa walimzuia kwa kumpiga risasi, na alipelekwa hospitalini; hali yake haijafahamika.

Hakuna afisa wa Secret Service aliyejeruhiwa.


Related Posts