Rais wa Russia, Vladimir Putin amekubali kwa kanuni pendekezo la kusitisha mapigano nchini Ukraine kwa muda wa siku 30 lililowasilishwa na Marekani, lakini ameweka masharti kadhaa.
Amesisitiza kuwa vipengele muhimu vinahitaji kujadiliwa zaidi ili kuhakikisha amani ya kudumu.
Masharti yaliyotolewa na Putin ni pamoja na Ukraine kutotumia kipindi cha kusitisha mapigano kujihami upya au kupokea msaada wa kijeshi kutoka mataifa ya Magharibi.
Mengine ni kutambuliwa kwa maeneo ambayo Russia imeyadhibiti kama sehemu yake na Ukraine kujiondoa katika azma yake ya kujiunga na Nato na kukubali hali ya kutofungamana kijeshi.
Aidha, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amekosoa msimamo wa Putin, akidai kuwa ni mbinu za kuchelewesha na kuweka vikwazo visivyokubalika kwa Ukraine.
Naye, Rais wa Marekani, Donald Trump, ameonyesha matumaini makini kuhusu kauli ya Putin, lakini amesisitiza haja ya mazungumzo zaidi ili kufikia makubaliano ya kina.
Endelea kufuatilia Mwananchi.