Na Mwandishi Wetu,Tanga
NAIBU Waziri wa Nishati Judith Kapinga amegawa mitun gi ya gasi 1500 kwa wakazi wa Kijiji cha Msomela Handeni Wilayani Handeni mkoani Tanga iliyotolewa na Kampuni ya Taifa Gas.
Kutolewa kwa mitungi hiyo kwa wakazi hayo inalenga kuunga mkono kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassani ya kumtua mzigo wa kuni Mama kwa kutumia nishati ya Taifa Gas na kuhifadhi Mazingira.
Akishukuru msaada huo Naibu Waziri wa Nishati Kapinga amesema Taifa Gas walichokifanya Msomela ni kupanda mbegu ya Mabalozi wa kudumu ambao watakuwa na wataendelea kuwa wateja wenu daima.
“Imarisheni huduma hii hapa Msomela na jirani kuzunguka Msomela ili wananchi hawa gesiikiisha wasipate tabu mahala pa kwenda kubadilisha.”
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Taifa Gas, Davis Deogratius amesema timu yake tayari imeshafanya mchakato wa kuwa na mawakala hapo Msomela tena wazawa, hivyo wasiwe na wasiwasi kwani gesi ikiwaishia wataipata Msomela na wale ambao hawajabahatika kupata mitungi ya Taifa Gas tayari ipo itakuwa inauzwa kwa bei nafuu.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando amewashukuru Taifa Gas kwa msaada mkubwa kwa Wananchi wake wa Msomela na aliendelea kuwaomba kuwa wananchi wake ni wengi hapa watapata nusu yao tu na nusu bado hivyo wakipata nafasi tena wasiwasahau Wananchi wa Msomela waliokosa.