Farida Mangube, Morogoro
Wafanyabiashara wa Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero, wamejitokeza kwa wingi kushiriki semina ya elimu ya kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Morogoro ikiwa na lengo la kuwambusha muhinu wa kulipa kodi
Akizungumza Katika Semina hiyo Meneja wa TRA Mkoa wa Morogoro, Bw. Sylver Rutagwelera,mesema semina hiyo ni sehemu ya utaratibu wa TRA wa kukutana na walipakodi kila Alhamisi ili kuwasikiliza, kutatua changamoto zao, na kupokea maoni yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Dunstan Kyobya ameiomba TRA kusogezea Huduma karibu kwani Halmashauri ya Mlimba imeendelea kukua kibiashara, lakini wafanyabiashara wanakabiliwa na changamoto ya umbali wa zaidi ya kilomita 100 kufuata huduma za TRA wilayani Kilombero.
“Hii ni changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wetu. Ni muhimu kwa TRA kufungua ofisi hapa Mlimba ili kuwasaidia wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali,” alisema Mhe. Kyobya.
Katika semina hiyo wafanyabiashara walipata fursa ya kuelewa wajibu wao wa kulipa kodi na kushiriki majadiliano ya wazi kuhusu changamoto wanazokutana nazo. Mwisho wa semina, washiriki walieleza kuridhishwa na mafunzo waliyoyapata na kuahidi kushirikiana na TRA katika kutekeleza wajibu wao wa kikodi.