Mshahara wa Chama kufuru nyie Yanga – Global Publishers



Kiungo mshambuliaji wa Mzambia, Clatous Chama

LICHA ya kusotea benchi katika kikosi cha kwanza cha Hamdi Maloud, unaambiwa kiungo mshambuliaji wa Mzambia, Clatous Chama analipwa mshahawa wa Dola 13, 000 (Sawa na Sh 34.3Mil) kila mwisho wa mwezi.

Mzambia huyo analipwa mshahara huo, mara baada ya kujiunga na timu hiyo, katika usajili wa msimu huu akitokea Simba kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika msimu uliopita.

Nyota huyo akiwa na msimu wake wa kwanza, ameonekana hana nafasi ya kudumu ya kucheza katika kikosi cha kwanza mbele ya Stephen Aziz Ki, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli.











Related Posts