Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha akizungumza katika kikao maalum cha watendaji wa Serikali na Barrick wanaosimamia zoezi la kufunga mgodi baada ya kutembelea eneo la Mgodi wa Barrick Buzwagi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha akizungumza katika kikao maalum cha watendaji wa Serikali na Barrick wanaosimamia zoezi la kufunga mgodi baada ya kutembelea eneo la Mgodi wa Barrick Buzwagi uliofungwa baada ya kumalizika muda wa uchimbaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha akizungumza katika kikao maalum cha watendaji wa Serikali na Barrick wanaosimamia zoezi la kufunga mgodi baada ya kutembelea eneo la Mgodi wa Barrick Buzwagi
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza katika kikao maalum cha watendaji wa Serikali na Barrick wanaosimamia zoezi la kufunga Mgodi wa Barrick Buzwagi
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza katika kikao maalum cha watendaji wa Serikali na Barrick wanaosimamia zoezi la kufunga Mgodi wa Barrick Buzwagi
Meneja wa ufungaji Mgodi wa Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi akizungumza wakati wa kikao hicho
Meneja Utekelezaji wa Mradi huo kutoka Barrick, Stanley Joseph akizungumza wakati wa kikao hicho
Wawekezaji 19 waanza shughuli za uzalishaji katika eneo hilo
**
Serikali imeridhishwa na mwenendo wa uanzishwa wa Kongani ya Buzwagi iliyopo katika manispaa ya Kahama, Mkoani Shinyanga katika eneo la Mgodi wa Barrick Buzwagi uliofungwa baada ya kumalizika muda wa uchimbaji na tayari wawekezaji 19 wamepatikana ambao miongoni mwao wameanza shughuli za uzalishaji katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha akiongea katika kikao maalum cha watendaji wa Serikali na Barrick wanaosimamia zoezi la kufunga mgodi baada ya kutembelea eneo hili, amesema licha ya zoezi kuendelea vizuri kasi kubwa inatakiwa kulikamilisha kabisa na kuwataka wadau wote kushirikiana katika hatua hii muhimu iliyobakia hususani kurekebisha baadhi ya miundombinu.
Amesema mradi mkubwa ni muhimu kwa maendeleo ya wilaya ya Kahama, Mkoa na taifa kwa ujumla kutoka na kuwa katika eneo lenye miundombinu mizuri ikiwemo uwanja wa ndege na barabara kuu ya kwenda nchi za Congo, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
Aidha amewaomba wawekezaji kuchangamkia fursa ya kuwekeza katika eneo hilo ambalo tayari lina miundombinu inayotakiwa katika Uwekezaji huku akiongeza kuwa ujenzi wa One Stop Center utafanyika haraka iwezekanavyo ili Wawekezaji wapate huduma zote zinazotakiwa katika uwekezaji sehemu moja ambapo kila mamlaka zitakuwa katika jengo moja.
Kwa upande wake Meneja wa ufungaji Mgodi wa Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi, amesema tayari eneo hilo la kongani ya Buzwagi limepatiwa usajiri na serikali kwa ajili ya shughuli hiyo ya Kongani
Mhandisi Mumbi, amesema kutoka na hali eneo hilo la kiuchumi la Kongani ya Buzwagi limeanza kuvutia wawekezaji na kwamba hadi sasa jumla ya wawekezaji 19 wamesajiriwa na mmoja kati yao tayari ameanza kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Kadhalika Mhandisi Mumbi amesema ili kuongeza ushawishi kwa wawekezaji wanatarajia kuanza kuitangaza Kongano ya Buzwagi kupitia majukwaa mbalimbali ya vyombo vya habari.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mboni Mhita amesema tayari Serikali imejipambanua kuhakikisha fursa zinazopatikana katika eneo hilo la Buwagi zinawanufaisha wananchi wa wilaya ya Kahama
Amesema ofisi yake kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imekutana na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa ajili ya kuwahamasisha kuwekezaji kwenye kongani ya Buzwagi na kuchangamkia fursa nyingine zikiwemo ujenzi huduma za kijamii kwa ajili malazi, chakula na vinywaji
Kwa Upande wake Meneja Utekelezaji wa Mradi huo kutoka Barrick, Stanley Joseph, amesema ana uhakika wadau wote katika Kamati ya uekelezaji wa kongani hiyo wakishiriana kwa karibu zoezi la kuikamilisha litafikiwa kwa haraka sambamba na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.
Maofisa kutoka Barrick wakiwa kwenye kikao