Serengeti Girls yaondoshwa kufuzu Kombe la Dunia

TIMU ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17, Serengeti Girls, leo jioni imeondoshwa kwenye mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia baada ya kukubali kipigo cha jumla ya mabao 4-0 dhidi ya Zambia.

Mchezo huo ulipigwa Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia ukiwa ni wa marudiano baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 nyumbani kisha kumaliziwa bao 1-0 ugenini.

Huo ulikuwa mchezo wa raundi ya pili na Serengeti Girls ilivuka baada ya Eswatini kujiondoa kwenye raundi ya kwanza ndipo ikakutana na Zambia.

Unakuwa msimu wa pili mfululizo timu hiyo inaondoshwa na Zambia kwenye mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia baada ya mwaka jana Serengeti Girls kukubali kichapo cha jumla ya mabao 5-1 baada ya kuanza kupokea kichapo cha mabao 5-0 Uwanja wa Nkoloma, Lusaka nchini Zambia, kisha kupata ushindi wa bao 1-0 nyumbani ambao ulizima matumaini ya kuendelea raundi ya tatu.

Related Posts