Bajana, Malckou wafanyiwa upasuaji, kukaa nje miezi minne

Klabu ya Azam FC imethibitisha kuwa itawakosa nyota wa kiungo mkabaji, Sospeter Bajana na beki wa kati, Malickou Ndoye kwa miezi minne baada ya kufanyiwa upasuaji wa majeraha yaliyokuwa yakiwasumbua.

Nyota hao wamefanyiwa upasuaji wa maungio ya mifupa ya nyonga ya kulia na kushoto (pubis symphysis), uliofanyika nchini Afrika Kusini katika Hospitali ya Life Vincent Pallotti jijini Cape Town.

“Kwa upasuaji huo, wachezaji hawa watakuwa nje kwa miezi minne kila mmoja, kuanzia siku ya upasuaji juzi Alhamisi ya Mei 16, 2024,” imesema taarifa ya klabu hiyo.

“Miezi mitatu ya kwanza itakuwa ya mazoezi tiba na mwezi mmoja wa mwisho utakuwa wa mazoezi ya utimamu wa miili.”

Related Posts