Majaliwa kuongoza kongamano wanahabari mitandao ya kijamii

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Zaidi ya washiriki 500 wanatarajia kushiriki katika kongamano la wanahabari wa mitandao ya kijamii litakalofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Kongamano hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (Jumikita) na Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (Tahliso) litafanyika Mei 20,2024 jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (Jumikita), Shaaban Matwebe, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la wanahabari wa mitandao ya kijamii litakalofanyika Dar es Salaam.

Akizungumza leo Mei 18,2024 na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Jumikita, Shaaban Matwebe, amesema lengo ni kujadili uandishi wa habari kupitia mitandao ya kijamii na upashanaji habari kupitia mitandao hiyo.

Amesema mada mbalimbali zitajadiliwa kama vile mitandao ya kijamii na uzalendo, fursa zilizopo kwenye tasnia hiyo, mafanikio na changamoto ili kutoa mchango wa uendeshaji kwa wadau kupitia Jumikita na mapendekezo yatakayosaidia serikali kwenye uratibu wa sera za jinsi ya kuunganisha sayansi ya uchumi wa taarifa.

Related Posts