
Hali ilivyo nyumbani kwa aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika, SP Awadh Mohamed Chiko Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
SP Awadh Chiko amefariki dunia jana majira ya asubuhi kufuatia ajali ya gari iliyotokea eneo la Pugu Sekondari, baada ya basi aina ya Eicher kugongana na gari lake la SP Awadh aina ya Prado, wakati akiwa akielekea katika majukumu yake ya kila siku.