Dar es Salaam. Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika jijini Dar es Salaam, SP Awadh Chico umeagwa leo Machi 18, 2025 na askari wenzake pamoja na ndugu jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo limeongozwa na Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP), Lucas Mkondya ambaye ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura.

Chico alifariki kutokana na ajali ilitokea saa 1:20 asubuhi jana Jumatatu, Machi 17, 2025 katika Barabara ya Nyerere maeneo ya Pugu, Mwisho wa Lami jijini Dar es Salaam ikihusisha gari aina ya Tata inayofanya safari zake kati Zingiziwa Chanika na Machinga Complex Ilala ikitokea Pugu kwenda Gongo la Mboto iligongana na gari ndogo aina ya Toyota Prado.
Endelea kufuatilia Mwananchi.