Trump Ni Janga Baya Kuliko Corona – Global Publishers



Rais wa Marekani, Donald Trump

Naibu wa Gavana wa Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya Luis de Guindos amesema kuwa, rais wa Marekani, Donald Trump amesababisha kukosekana utulivu katika ghughuli za kiuchumi na rais huyo ni janga baya zaidi kuliko hata janga la Corona la miaka mitano iliyopita.

Shirika la Habari la IRNA limemnukuu Luis akisema hayo katika mahojiano na gazeti la Uingereza la Sunday Times na kuongeza kwamba, siasa mbaya za ushuru za Trump, mipango yake ya kufuta mfumo wa kifedha na kutia mkono mfumo wa kodi ya makampuni na mashirika mbalimbali, imeleta mabadiliko ya haraka katika masoko na kutatanisha utabiri wa kupambana na mfumuko wa bei na riba.

Ameongeza: “Lazima tuseme kwamba, kukosekana utulivu katika sasa ni janga kubwa zaidi kuliko la Corona. Utawala mpya wa Marekani haujali ushirikiano wa pande nyingi, ushirikiano kati ya nchi na wala kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa matatizo ya wote. Haya ni mabadiliko makubwa sana na ni chanzo cha ukosefu mkubwa mno wa utulivu.”

Naibu wa Gavana wa Benki Kuu ya Ulaya pia ameviita vita vya biashara kuwa havina mshindi bali kila mtu anapoteza na ameilaumu Marekani kwa kuanzisha vita hivyo na kusababisha pande nyingine nazo zichukue hatua za kulipiza kisasi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio juzi alisema kwamba baada ya Marekani kuziongezea ushuru bidhaa za washirika wake wakuu wa kibiashara sasa inaweza kuingia katika mazungumzo na pande hizo kuhusu uhusiano mpya wa kibiashara baina yao.


Related Posts

en English sw Swahili