Mastaa wafunika Ramadhani Star Ligi

Wachezaji watatu, Fotius Ngaiza, Omary Sadiki na Jimmy Brown walikuwa kivutio, katika mashindano ya Ramadhani Star Ligi kutokana na uwezo wao.

Ngaiza anayecheza nafasi ya namba 5 ‘Centre’,  aliyechezea Soud Black  na alionyesha uwezo mkubwa wa kudaka mipira yote ya ‘rebound’ na kufunga.

Katika mchezo huo na Team Mkosa aliongoza kwa kudaka mipira ya ‘rebound’  mara 15  na kufunga pointi 17.

Kwa upande wa Sadiki anayecheza namba 1 ‘Point Guard’ Soud Black alionyesha uwezo mkubwa akiwaunganisha vizuri  wachezaji wake pamoja  asisti zake alizokuwa anatoa.

Katika mchezo wao na Team Mkosa alitoa  asisti  12,  na  kufunga pointi 15. 

Brown anayecheza namba 4 ‘Power forward’ Team Mkosa, ubora  alioonyesha katika mchezo wao,  aliongoza kwa upande timu yake kudaka mipira yote ya ‘rebound’ akifanya hivyo mara 10 10, na alizuia mara ‘block’  mara tano.  

Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Soud Black iliishinda Team Mkosa  kwa pointi 57-50.

Mchezo mwingine Team Mngeja iliishinda Team  Labani kwa pointi 41-37.

Katika mchezo huo Team Mngeja iliongoza katika robo mbili za kwanza kwa pointi 8-7 na 24-12, robo ya tatu Team Labani iliongoza kwa pointi 7-5 na 11-4.

Ramadhani star Ligi imeandaliwa na taasisi  ya kituo cha Mchezo cha Mchenga Academy na inashirikisha timu nane zilizopewa majina ya wachezaji hao nyota.

Timu zinazoshiriki ziligawanywa katika makundi mawili,  kundi A ilipewa jina la Team Miyasi, Mwalimu, Nahreel na Evance, huku kundi B  ni  Team Soud Black, Amin Mkosa, Mngeja na Labani.

Katibu  Mkuu wa ligi hiyo, Isakwisa Mwamusope  alisema bingwa wa mashindano hayo atapata Sh3 million na ya pili itapewa Sh1.5 milioni.

Msanii Emmanuel Mkono wa ‘Nahreel’  ndiye aliyekuwa kivutio katika mchezo wao dhidi ya Team  Miyasi.

Msani huyo aliyeichezea Team Nahreel anacheza  namba  1  ‘Point Guard’, na alionyesha uwezo kwa kumiliki eneo la katikati pamoja na asisti alizokuwa anatoa.

Nahreel alitoa asisti tano na kufunga pointi nane licha ya kufungwa na Team Miyasi  kwa pointi 40-28.

Julias John kocha kutoka Temeke, alisema msanii  huyo ana uwezo mkubwa  wa kucheza mchezo wa kikapu.

“Kama angepata ushirikiano mzuri na wachezaji wenzake, naamini timu yake ingeshinda,” alisema John.

Related Posts