Kamishina wa ufundi na mashindano wa Ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salam (BDL), Haleluya Kavalambi amesema ligi hiyo inatarajiwa kuanza mwezi Aprili na tarehe kamili itatangazwa baada ya kikao cha kwanza cha BD na klabu kufanyika.
“Kikao hicho kitazungumzia mapitio ya kanuni na kuzipitisha, ambazo ndizo zitakazoongoza na kusimamia msimu wa Ligi ya 2025,” alisema Kavalambi.
Alitaja timu zitakazoshiriki upande wanaume ni JKT, UDSM Outsiders, Dar City, ABC, Chui, DB Oratory, KIUT, Mgulani JKT, Vijana ‘City Bulls’, Srelio, Savio, Mchenga Star, Pazi, Polisi, Stein Warriors na Kurasini Heat.
Kwa upande wa timu za wanawake ni DB Lioness, Vijana Queens, JKT Stars, Jeshi Stars, Polisi Stars, Tausi Royals, UDSM Queens, DB Troncatti, Pazi Queens na Twalipo Queens.
“Timu za wanawake ambazo, zinataka kushiriki ligi ya mkoa wa Dar es Salaam, zinatakiwa kutuma uthibitisho kwa maandishi na kuwasilisha barua kwa mkurugenzi wa ufundi na mashindano wa BD,” alisema Kavalambi.