MAPINDUZI MAKUBWA MSD MIAKA MINNE YA RAIS DKT SAMIA MADARAKANI

Mkurungenzi wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), Mavere Tukai amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu amefanya mapinduzi makubwa ya uwekezaji katika sekta ya afya na kuiweka nchi katika viwano vya kimataifa husasani katika utendaji wa Bohari ya Dawa (MSD)

Tukai amesema hayo leo Jumatano Machi 19, 2025 alipokuwa akizungumzia mafaniko ya miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suliu Hassan tangu aingie madarakani katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),jijini Dodoma ikiwa ni utaratibu uliowekwa na ofisi ya Msemaji wa Serikali.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Tukai, tangu Rais Samia aingie madarakani amewezesha upatikanaji wa bidaa za afya na hadi kufikia mwaka huu, jumla ya bidhaa asiria 382 zilisambazwa kutoka 290 za awali sawa na ongezeko la asilimia 42 mwaka 2021/22 hadi asilimia 67 mwezi Februari 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 23.

“Lengo letu ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha 2054/2025 tufike asilimia 80 mpaka 90 na kwa mwendo huu tunaoenda nao hilo linawezekana kwani sasa tumeshavuka lengo.

” Alisema kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Samia, MSD imefanya manunuzi na usambazaji wa vifaa na vifaa tiba vinavyohitajika katika vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi vituo vinavyotoa huduma za kibingwa na ubingwa bobozi nchini.

Alisema baadhi ya vifaa vilivyosambazwa ni pamoja na mashine za usingizi, CT-Scan, MRI 3T, Utrasound na Digital X-Ray vyenye thamani ya Sh376. 6 bilioni.

Akizungumzia uwekewazaji uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Mkurugenzi Mavere alisema MSD inajivunia kwa kuwezesha maono ya Rais Samia ya kupunguza vifo hivyo hadi kufikia 104 vya sasa kutoka 556 vilivyokuwa vikitokea awali na kuwezesha kiongozi huyo kutambulika kimataifa na kupewa Tuzo.

“MSD jukumu letu lilikuwa ni kupeleka vifaa tiba, tumetekeleza kwa asilimia 100 katika miradi ya unuinuzi wa vifaa vya dharura , uzazi pinamizi na huduma za watoto wachanga (CE)mONC) ambako vituo 316 vya kutolea huduma za afya vilinufaika kwa Sh100 bilioni.
Mpaka sasa usambazaji huo umefikia asilimia 100,” aliisisitiza Tukai.

Tukai alisema fedha zote zilizowekezwa katika kipindi kifupi cha miaka minne zinalengo la kuboresha huduma ya afya kwa wananchi. Kwa upande wa miradi inayohusisha magonjwa ya TB, HIV na Malaria, Mkurugenzi Tukai alisema kwa kipindi cha mwaka 2021 mpaka 2023 MSD imefikia asilimia 95 ya malengo.

Kuhusu usambazaji wa vyandarua ili kujinga na ugonjwa wa maralia Tukai alisema jumala ya vyandarua milioni 7.2 vilisambazwa. “Mwaka 2023/2024 tulisambaza vyandarua milioni tisa sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 30.

Alisema kuhusu vifaa tiba mwaka 2020 jumla ya Sh18 bilioni zilitumika na mwaka uliofuatia zilitumika Sh56 bilioni wakati mwaka 2024 jumla ya Sh93 bilioni zilitumika.

” Hivi tunavyoongea yaani mwezi Machi , tayari zimeshatumika Sh109 ikiwa bado miezi kadhaa kabla ya kumaliza mwaka wa fedha wa 2024/25.

Tukai alisema mafanikio yote hayo yametokana na uwekezaji wa Serikali chini ya Rais Samia na kwamba MSD wanapotumwa wanatekeleza kwa lengo la kuwapa huduma bora wananchi.

“MSD pia imeboresha upatikanai wa huduma bora ya kinywa na meno kwa kununua viti vya kinywa na meno 693 pamoja na mashine zake za mionzi 533 kwa gharama ya Sh13 bilioni,”amesema.

Alisema sasa huduma hiyo imesogezwa karibu na wananchi zikiwa na ubora unaokubalika kuanzia ngazi ya kituo cha afya, wilaya, mkoa, rufaa mpaka Taifa.

 

Related Posts