BAADA ya dakika 90 Kwenye Kariakoo Dabi ya Wanawake kukamilika na ubao kusoma Simba Queens 0-1 Yanga Princess rekodi ya timu hiyo kutopoteza pointi tatu ndani ya msimu wa 2024/25 imeyusha mazima na watani zao wa jadi.
Ikumbukwe kwamba baada ya Simba Queens kucheza mechi 12 ilikuwa haijapoteza mchezo ndani ya ligi kwenye dakika 1,080 mchezo wake wa 13 ilikuwa ngoma nzito kuendeleza rekodi hiyo wakibakiwa na pointi 34 kibindoni na kushushwa nafasi ya kwanza na JKT Queens.
Machi 18 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC, Comple x ulisoma Simba 0-1 Yanga na mechi nyingine zilizochezwa kwenye Ligi ya Wanawake ilikuwa Alliance Queens 1-0 Gets Program, Mlandizi Queens 2-5 Ceasiaa Queens.
Kwenye mechi 13 ambazo imechezwa kwa sasa ni ushindi katika mechi 11, sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja, safu ya ushambuliaji imetupia mabao 43 huku ukuta ukiwa umeruhusu kutunguliwa mabao 8.
Ushindi wa mabao 5-0 walipata JKT Queens Machi 19 2025 dhidi ya Mashujaa Queens mchezo uliochezwa Uwanja wa Isamuhyo unawapa tiketi ya kukaa nafasi ya kwanza ikiwa nit imu pekee ambayo haijapoteza ndani ya ligi kwenye mechi 13 ambazo imecheza na pointi zake kibindoni ni 35.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.