Kikosi cha Yanga Kuifuata Singida Black Stars Kesho – Global Publishers



INAELEZWA kuwa msafara wa Yanga unatarajiwa kuondoka Jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi kwa Treni ya SGR hadi Mkoani Dodoma kisha utapanda basi kuelekea Singida.

Msafara huo unakwenda huko kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa uzinduzi wa Uwanja wa Singida Black Stars uliotengenezwa kwa kupitia Makampuni mbalimbali utakaotumika kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu Bara.

Uwanja huo unatarajiwa kuzinduliwa Jumatatu ijayo kwa mchezo wa kirafiki kati ya Singida Black Stars dhidi ya Yanga huku Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ ambaye ndiye mgeni rasmi.











Related Posts