Chelsea ya wanawake yatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England
BAO la dakika 90 lililowekwa kimiani na Salum Akida Shuruku lilimeiwezesha watetezi wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), KMKM kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Malindi na kufufua matumaini ya kutetea taji hilo inalolishikilia kwa misimu mitatu mfululizo tangu mwaka 2021.
Ushindi huo uliopatikana kwenye Uwanja wa Amaani Kwa Wazee, mjini Unguja umeifanya KMKM kufikisha pointi 48 na kuchupa kutoka nafasi ya tano iliyokuwapo awali hadi ya pili nyuma ya JKU inayoongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 53 kila moja ikicheza mechi 24 hadi sasa.
Malindi iliyotoka kupoteza pointi tatu na mabao mawili mezani mbele ya Chipukizi baada ya kuadhibiwa na ZFF kutokana na fujo ilizofanya visiwani Pemba, ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao lililowekwa wavuni na Omar Thani Abdalla dakika ya 34.
Hilo lilikuwa ni bao la nane kwa nyota huyo aliyetua Malindi katika dirisha dogo akitokea Ngome.
Hata hivyo, bao hilo lilisawazishwa na KMKM katika dakika ya 45, sekunde chache kabla ya mapumziko kupitia kwa Firdaus Seif Amour, likiwa ni bao la tatu kwake kwa msimu huu.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji, lakini ni KMKM ndio iliyonufaika baada ya kupata bao la pili na la ushindi, lililowekwa wavuni na Salum Akida Shukuru dakika 90 linalomfanya nyota huyo kufikisha jumla ya mabao matano hadi sasa kwa msimu huu.
Kipigo hicho ni cha 12 kwa Malindi na kimeiacha timu hiyo katika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 29 kama ilizonazo Uhamiaji na Ngome, inazotofautiana nazo mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mchezo mwingine uliopigwa kwenye Uwanja wa Mao A, eneo la Kikwajuni Juu mjini Unguja, Kundemba iliendelea kuokota pointi baada ya kuinyoa Hard Rock kwa bao 1-0 na kuifanya ifikishe alama 23 ikisaliwa nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi 25.
Bao lililoipa Kundemba ushindi jioni ya leo liliwekwa kimiani na Fahmi Salum Mussa katika dakika 76 likiwa ni la tatu kwa mchezaji huyo kwa msimu huu.
Matokeo ya mechi hizo za leo yanazidi kufanya mbio za ubingwa kunoga, kwani sasa JKU inatofautiana na KMKM kwa pointi tano, huku KMKM ikitofautiana pointi moja tu na KVZ na Zimamoto zinazokamilisha Nne Bora, kwani kila moja ina pointi 47, japo Zimamoto imecheza mechi 23 tu.
Mbali na ushindani uliopo katika mbio za ubingwa wakati ligi ikiwa imesaliwa na mechi zisizozidi sita, hata eneo la mkiani nako kuna timu zinapambana na hali zao ili kuepuka kushuka daraja ikiwamo Maendeleo inayozibeba timu zote ikiwa na pointi 15 tu hadi sasa ikicheza michezo 24.
Timu nyingine zilizopo kwenye mstari mwekundu na kuhitajika kufanya kazi ya ziada kwa mechi ilizonazo mkononi kabla ya msimu kufungwa rasmi katikati ya Juni ni Jamhuri ya Pemba yenye pointi 18, ikiwa nafasi ya 15, Ngome yenye pointi 20 na Kundemba yenye alama 23.
Kwa mujibu wa kanuni ya Ligi Kuu Zanzibar, timu nne za mwisho katika msimamo zinashuka moja wa moja kwenda Ligi Daraja la Kwanza Taifa.
Ngome ni kati ya timu nne zilizopanda daraja msimu huu sambamba na New City, Chipukizi na Maendeleo, zilizochukua nafasi ya Black Sailors, Polisi, Taifa Jang’ombe na Dulla Boys zilizoshuka msimu uliopita kwa kushika nafasi nne za chini za msimamo mabingwa wa kihistoria, KMKM.simu ulioisha.