Arusha Food Systems Youth Leaders waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula Mashuleni

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula Mashuleni Arusha Food Systems Youth Leaders   wametembelea shule ya sekondari Ungalimited na kutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na walimu kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira kwa ajili ya kuwa na mifumo endelevu ya chakula ikiwemo kupanda miti ya matunda.

Viongozi vijana wa mifumo ya chakula Arusha, wanafunzi pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari Ungalimited wameweza kupanda miti ya matunda katika shule hiyo takribani miti 50 ambayo ni mipapai 10, miembe 10, mipera 10, michungwa 10 na matopetope 10.

Pamoja na kupandaji miti vijana hao walifanikiwa kuzungumza na wanafunzi kuhusu umuhimu wa elimu katika maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla pamoja na faida za kupanda miti ya matunda kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira na kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora kwa kizazi cha sasa na cha baadae.

Jumla ya wanafunzi 1376 na walimu 7 wameshiriki kikamilifu katika zoezi la kupanda miti na kujifunza mbinu za kuitunza miti hiyo hadi itakapozaa matunda ambapo uongozi wa shule hiyo uliunga mkono mpango huu na kuahidi ushirikiano zaidi katika siku zijazo. Pia uongozi wa shule uliomba kuongezewa idadi ya miti ya matunda na kuanzishiwa bustani ya mbogamboga.

Shughuli hii imekuwa na mafanikio makubwa, ikionyesha nguvu ya vijana katika kusukuma mbele mifumo endelevu ya chakula na utunzaji wa mazingira. Hivyo AFSYL inatarajia kuendelea na juhudi hizi ili kuongeza community impact kwa siku zijazo.

Related Posts