ASA kuanza kukabiliana na tindikali ya afya ya udongo

Wakala wa Mbegu za kilimo ASA inatarajia kuanza kutibu Udongo kwa Mashamba yake yenye upungufu wa virutubisho vya Udongo.

 

Hayo yamsemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt. Sophia Kashenge wakati akifunga mafunzo ya Udhibiti ubora wa Mbegu za kilimo Kwa watumishi wa ASA 31 katika shamba la Mbegu Dabaga kilolo Iringa.

Mafunzo hayo ya kiratibiwa na Taasisi ya Udhibiti ubora wa Mbegu Nchini TOSCI kupitia Mradi wa kuboresha Tasnia ya Mbegu Nchini (ESSETA) unaofadhiliwa na BMGF chini ya usimamizi wa AGRA.

 

Dkt. Sophia amesema ilikufikia Malengo ya uzalishaji wa mbegu Wakala umeanza hatua za awali za kutibu Udongo ilikuondoa Tindikali ya Udongo hatua ambayo itasaidia kuongeza tija ya Uzalishaji wa Mbegu.

Amesema katika uwekezaji uliopo Wakala umenunua mashine za kupimia Udongo (Soil scanner) ambazo zimeanza kufanya kazi katika Mashamba ya Wakala ilikubaini hali halisi ya Afya ya udongo hasa uwepo wa Tindikali hiyo.

Amesema kwa sasa wakala utakuwa unafanya zoezi kubwa la kupima Afya ya Udongo wa Mashamba yake kila mwanzo wa msimu ili kubaini changamoto za Afya ya Udongo na kuweza kujua mbolea Gani inapaswa kutumika kwa wakati huo.

Related Posts