Wananchi watakiwa kuepuka mikopo yenye masharti magumu kutoka kwa matajiri matapeli

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Kanali Denis Mwila amwataka wananchi kuepuka mikopo yenye masharti magumu yanayowaumiza watu wa hali ya chini inayotumiwa na baadhi ya matajiri wanaojihusisha na kilimo cha mpunga katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Kanali Mwila amesema hayo wakati wa mkutano wa ugawaji hatimiliki za ardhi za wakazi wa viijiji vya Lujewa, Ubaruku na mpakani vya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya waliomilikishwa na mradi wa Urasimishaji Makazi unaotekelezwa na Chuo Kikuu Ardhi kwa usimamizi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Amesema kumekuwa kuna tabia ya baadhi ya Matajiri wanaokopesha wananchi fedha kwa malipo yenye masharti magumu, lakini kwa sasa kwakuwa wananchi hao wamepewa hati za kumiliki ardhi zitawasaidia kuiinua kiuchumi kwa kutumia kama dhamana katika mabenki yaliyo rasmi na yenye mikopo ya masharti nafuu.

Aidha, amesema kwa sasa imefikia hatua mwananchi anakopeshwa shilingi 2,000,000 ndani ya miezi minane anatakiwa kulipa shilingi 15,000,000 au nyumba yake iuzwe kufidia deni.

Akatoa pia mfano mwingine wa mkopo wenye masharti magumu ambapo mkopaji anakopeshwa shilingi 100,000 halafu anarejesha magunia matatu ya mpunga ndani ya miezi nane ambapo kuna muda gunia moja linauzwa mpaka shilingi 450,000.

Nao baadhi ya wananchi wa walipewa hati Bw. Wille Mwandumbya, Bibi Adjentina Mjungwa na Joyce Nziku wameahidi kutumia hati hizo katika kujiinua kiuchumi hasa kuzitumia kama dhamana katika taasisi za fedha ili kujipatia mikopo mbalimbali.

Related Posts