WADAU WA MADINI WAENDELEA KUNUFAIKA NA MNADA WA MADINI ARUSHA

– Wauzaji wapata fursa ya kuuza madini

– Wafanyabiashara wapata fursa ya kuona madini mbalimbali.

– Kuuzwa kwa bei ya ushidani

Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, CPA. Venance Kasiki amesema, wafanyabiashara wa madini wamepata fursa ya kuleta na kuangalia madini mbalimbali katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) ikiwa ni sehemu ya kuelekea siku ya mnada wa pili wa madini ya vito unaotarajiwa kufanyika Jijini Arusha siku ya Jumanne ya Aprili 8, 2025.

CPA. Kasiki amesema hayo leo Aprili 7, 2025 wakati wa zoezi la kuangalia na kukagua madini linalofanyika kwa siku tatu kuanzia Aprili 5 hadi Aprili 7, 2025 kabla ya madini kwenda kuuzwa kwa bei ya ushindani siku ya tareh

Amesema mnada huo utafanyika kwa njia ya mtandao ambapo wafanyabiashara watapata fursa ya kushindana kwa bei ambapo atakayekuwa na kiwango cha juu kinachokubalika na muuzaji ndiye atakayeuziwa madini hayo na kukabidhiwa baada ya kukamilisha taratibu zote za manunuzi.

“Siku ya mnada hakutakuwa na madini eneo la tukio mnada utakuwa wa mtandaoni kila mtu ataona madini na bei husika,” amesema Kasiki.

Ameongeza kuwa baada ya Arusha mnada huo pia utafanyika katika mikoa mingine yanapopatikana madini ya vito ambayo ni Morogoro, Ruvuma, Tanga, Mahenge, Dar es salaam na Lindi.

Kwa upande wake Afisa Biashara Mwandamizi kutoka Soko la Bidhaa Tanzania, Nicolaus Kaserwa amesema kuwa lengo la kufanya biashara mtandaoni ni kuwa na uwazi, ushindani na kupunguza gharama kwa wateja pamoja na kuongeza wigo wa soko kwa wafanyabiashara.

Amebainisha kuwa baada ya mafanikio ya mnada wa kwanza, maboresho makubwa yamefanyika kuelekea katika mnada wa pili kwa kuzingatia maoni ya wadau na kuwataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha mnada huo.

Naye mmoja wa wafanyabiashara wa madini ya vito, Kalanga Mokoyo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kufanikisha uhakika wa upatikanaji wa masoko kupitia minada ambayo inatoa fursa katika kuuza na kununua madini kwa uwaz

“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka hii minada ambayo inaturahisishia kupata madini kwa wakati ni mtaji wako tu, pia mnada huu unatutoa wasiwasi, zamani ilikuwa tukisikia tunajificha tunaogopa kumbe ni tofauti sasa hivi kila kitu kipo wazi tunashiriki na tunanunua kiurahisi,” amesema Mokoyo.





Related Posts