Serikali kuwafagilia njia wawekezaji sekta ya mawasiliano

 

SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya wawekezaji ili kuongeza chachu katika maendeleo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea). 

Hayo yalibainishwa mwisho mwa wiki iliyopita tarehe 17 Mei 2024, na Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano, Nape Mnauye wakati akishuhudia makubaliano ya Kampuni ya Towerco of Africa na British Internation investment ya kujenga miundombinu ya mawasiliano nchini.

“Leo tumeshuhudia makubaliano ya uwekezaji miondombinu ya mawasiliano wenye thamani ya Dola Sh. 30 milioni katika ya Kampuni ya Towerco of Africa na wenzetu wa British Internation investment wamekuja kuwekeza kwenye sekta yetu hii,” alisema Nape.

Alisema kuwa uwekezaji huo umefanyika wakati muafaka kwa kuwa umeendana na bajeti.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

Haya ni mafanikio makubwa na hasa tukizingatia tumepitisha bajeti jana tumeona ujio wa sekta binafsi katika kuongeza nguvu kwenye uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano.

Waziri Nape alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita inaendelea kujenga mazingira bora zaidi kwa uwekezaji.

“Uwekezaji huu utakwenda kuongeza nguvu katika mapinduzi ya nne ya viwanda kwenye nchi yetu tunayoendeleo nayo nipo hapa kuthibitisha utayari wa serikali kuendea kujenga mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuwekeza nchini kwetu,” alisema Waziri Nape.

Kwa upande wake, Innocent Mushi, Mkurugenzi wa Towerco of Africa amesema kuwa kampuni hiyo na Britishi Internation Investment imesaini makubaliano ya kujenga miundombinu ya mawasiliano.

“Sisi Towerco na British Internation investment tumasaini kiasi cha dola za kimarekani 30 milioni kwa ajili kuwekeza kujenga miondombinu ya minara hususani vijijini kwa ajili ya kuwawezesha watoa huduma za mawasiliano kufanya shughuli zao,” alisema Mushi.

Alisema kuwa dhamira ya Towerco ni kama dhamira ya Serikali kuhakisha kuwa watu wote wanaunganisha na mawasiliano. “Uwekezaji huu utatimiza adhma ya Serikali na Dunia kwamba watu wote waweze kuunganishwa kwenye mtandao”

Alisema kuwa kampuni hiyo inatarajia kujenga minara takribani 200 kwa mwaka 2024

Mushi alisema kuwa uwekezaji huu utazingatia utunzaji wa mazingira ili kuhakikisha kuwa nchi inakuwa salama

Related Posts