WADAU WA USAFIRI KUKUTANA KUJADILI UFUMBUZI WA CHANGAMOTO ZA MADEREVA


*****

Taasisi ya Huduma yangu Faoundation imeaanda Bodoboda Bajaj Summit kongamano lengo la kukutanisha wadau wa usafiri kutoa serikali na sekta ya binafsi kujadili kwa pamoja namna ya kutatua changamoto zinazo wakabili madereva waenda bodaboda na bajaji nchini. 

 Akizungumza na waandishi habari ,Mkurugenzi Taasisi ya Huruma Yangu Foundation, Esta Richard amesema kongamano hilo litafanyika Aprili 10 katika chuo kikuu cha mlimani jijini Dar es salaam ambapo litahusisha wadau wote wa bodaboda na Bajaji, Polisi trafic pamoja na watu kutoka hospital ya Muhimbli. 

 Ameongeza kuwa kongamano la Bodaboda bajaj summit itakutanisha serikali, Tasisi binafsi, taasis za afya Latra na TRA kuelezea namna gani wameweka mifumo kwenye kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya usafiri ikiwemo waendesha boda na bajaji. 

 “Tunategemea kupata matokeo mbalimbali kutoka na huu mdahalo na tunategemea kuanzisha jukwaa ambalo litamkutanisha dereve boda boda boda na wadau wote wanaohusika kwenye sekta ya usafirishaji hapa tanzania ili kuweza kutatua changamoto” amesema Richard 

 Aidha amesema matengemeo yao kutoka kwenye kongamano hili ji kuweza kutatua changamoto ya ajali za kati dereva na abiria na kufanya kijana anaejihusisha na kazi bodaboda na bajaji kupata elimu ya fedha na kujua kupanga matumizi ya maendelo yake ya baadae 

 Awali akizungumza Mrakibu mwandimizi kutoka Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani, Mbunja Matibu amesema jukumu lao kubwa kwenye mkutano huo ni kutoa elimu kwa bodaboda na bajaji ili kuhakikisha wanafata sheria za usalama barabarani ili kujinusuru na ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara. 

 Tunawakumbusha uvaaji wa kofia ngumu element, endapo utapata ajali sehemu ya kichwa sehem mbaya sana kwa ajali, kutopakia abairia zaidi ya mmoja itasaidia kupunguza vifo kwenye ajali pindi napotokea” amesema Mrakibu Matibu

Related Posts