SERIKALI YASHUHUDIA MKATABA WA USD MILIONI 30 KUJENGA MINARA TANZANIA KATI YA TOA TANZANIA NA BII

Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye(katikati) na balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Divid Concar (Kulia) wakishuhudia Mtendaji Mkuu wa TOA Tanzania Innosent Mushi wapili kushoto na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa British International Investment Sithembumenzi Vuma (wapili kulia) wakibadilishana hati za mikataba wa kuboresha huduma za mawasiliano nchini. Katika mkataba huo British International Investment imetoa kiasi cha USD milioni 30,kwa TOA kwa ajili ya kujenga Minara 200 ili kuweza kuongeza upatiakanaji wa huduma za mawasiliano Vijijini. Hafla hiyo ya utiwaji saini imefanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Moses Nape Nnauye(katikati) na balozi wa Uingereza hapa nchini Divid Concar (Kulia) wakifurahia baada ya Mtendaji Mkuu wa TOA Tanzania Innosent Mushi (kushoto) na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa British International Investment Sithembumenzi Vuma (wapili kulia)kumaliza kusaini hati za mikataba ya kuboresha huduma za mawasiliano nchini. British International Investment imetoa kiasi USD milioni 30,kwa TOA Tanzania kwa ajili ya kujenga Minara 200 ili iweze kuongeza upatiakani wa huduma za mawasiliano Vijijini hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Moses Nape Nnauye akiongea wakati wa hafla ya British International Investment kuikabidhi TOA Tanzania kiasi USD milioni 30 kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu ya mawasiliano na kuboresha huduma za mawasiliano nchini fedha hizo zitatumika kujenga Minara 200 ili kuongeza upatiakani wa huduma za mawasiliano Vijijini, Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa British International Investment Sithembumenzi Vuma akizungumza wakati hafla ya kusaini mkataba wa kuboresha huduma za mawasiliano nchini. British International Investment imetoa kiasi cha Dora za Kimarekani milioni 30,kwa TOA kwa ajili ya kujenga Minara 200 ili kuweza kuongeza upatiakanaji wa huduma za mawasiliano Vijijini hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya TowerCo of Africa Tanzania (TOA Tanzania), imesaini makubaliano na taasisi ya Uingereza, British International Investment (BII) ya kiasi cha USD Milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa kupanua miundombinu ya mawasiliano nchini Tanzania

Fedha hizo zilizotolewa na BII zitaiwezesha TOA kujenga minara mipya 200 nchini na kufanikisha adhma yake ya kuongeza ujumuishi wa kidijitali Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano hayo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, waziri wa Habari Teknolojia na Mawasiliano Nape Nnauye amepongeza hatua ya uwekezaji huo wenye tija nchini na kusema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya wawekezaji ili kuongeza chachu katika kukuza maendeleo ya nchi yetu.

“Leo tumeshuhudia makubaliano ya uwekezaji mkubwa wa miondombinu ya mawasiliano wenye thamani ya USD milioni 30 katika ya Kampuni ya Towerco of Africa na Wenzetu wa British Internation investment, uwekezaji huu umefanyika wakati muafaka kwa kuwa umeendana na bajeti .

Amesema hayo ni mafanikio makubwa kwani uwekezaji huo utakwenda kuongeza nguvu katika mapinduzi ya nne ya viwanda nchini yanayoendelea ma kwamba serikali ipo tayari kuendea kujenga mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuwekeza nchini kwetu.

Kwa upande wake Innocent Mushi Mtendaji Mkuu wa TOA Tanzania amesema minara hiyo mipya 200 itakayojengwa kutokana na makubaliano waliyosaini utasaidia kuongeza upatikanaji wa mawasiliano Tanzania Bara na Visiwani na hivyo kuwaungasnisha watanzania wengi zaidi ambao walikua mbali na huduma ya mawasiliano.

“Makubaliano haya ya uwekezaji wa fedha na BII yatatuongezea nguvu ya kufikia malengo yetu ya kupanua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuongeza kasi ya kukua kwa huduma za kidijitali Tanzania”. Amesema Mushi.

Amesema, dhamira ya Towerco ni kama dhamira ya Serikali kuhakisha kuwa watu wote wanaunganisha na mawasiliano. “Uwekezaji huu utatimiza adhma ya Serikali na Dunia kwamba watu wote waweze kuunganishwa kwenye mtandao”

Ameongeza kuwa, sasa wanaweza kukuza upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kimtandao kwenye jamii zilizokuwa mbali na huduma hizo na kujidhatiti kwenye mazingira endelevu na maendeleo ya jamii.

Amesema utengenezaji wa saiti hizo mpya utazingatia utunzaji wa mazingira, matumizi ya nishati jadidifu na utupaji wa taka salama ili nchi kuwa katika mazingira yake mazuri.

Naye, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar, ameeleza kufurahishwa kwake na makubaliano hayo ambayo yataenda kupanua huduma za mawasilinao chini.

“tumefurahi kushuhudia utiwaji sainiwa wa makubaliano haya muhimu kwa BII ambayo yatawezesha upanuzi wa huduma za mawasiliano na kufikia watanzania wa maeneo hadi ya vijijini.

Related Posts