****
Rais Mstaafu wa Tanzania na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasilisha Ujumbe Maalum ambao ulipokewa na Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Guinea ya Ikweta, Mhe. Simeon Oyono Esono Angue, kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo, Mhe. Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.
Uwasilishaji wa ujumbe huo ulifanyika katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini Malabo tarehe 13 Aprili 2025.