…………….
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema
Vyombo vya habari vimechangia katika utekelezaji wa 4R za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwa ni sekta muhimu katika kupeleka ujumbe kwa jamii.
Aidha, Prof. Kabudi amewataka Wanahabari kufanyakazi kwa kuzingatia maadili , Uhuru na taratibu za taaluma hiyo ili kupunguza changamoto zinaweza kujitokeza katika jamii kutokana na mgongano wa kimaslahi
Prof. Kabudi ameyasema hayo leo Jumatatu Aprili 14,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Sambamba na hilo ameongeza kuwa Wizara imefanikiwa kuleta utulivu kwenye sekta ya habari ambapo vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungiwa kwa Makosa mbalimbali vilifunguliwa na Wizara imekuwa na mweleke wa kuvilinda vyombo vya habari Hali iliyosababisha kuogezeka kwa uhutru wa vyombo vya habari.
Waziri Kabudi amesisitiza kuwa uhuru wowote una mipaka hakuna uhuru ambao hauna mipaka kwani Uhuru ambao hauna mipaka ni fujo.