UCHUKUAJI FOMU ZA UBUNGE CCM RASMI JUNE 28


 ****

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kwamba baada ya mashauriano na Wanachama wake, kutafakari na kupima kwa umakini ushauri huo, kimeamua kufanya marekebisho juu ya ratiba ya mchakato wa ndani wa uteuzi wa Wagombea wa nafasi ya ubunge, ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na udiwani, kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi usiku huu imesema “Kwa kuzingatia marekebisho hayo, sasa mchakato huo, utaanza rasmi tarehe 28 Juni 2025, saa 2:00 asubuhi na kukamilika tarehe 2 Julai 2025, saa 10:00 jioni, kwa kufuata utaratibu ule ule uliotangazwa kwenye taarifa ya tarehe 10 Aprili 2025”

Itakumbukwa awali Chama Cha Mapinduzi kiliwatangazia Wanachama wake kwamba, mchakato wa ndani ya Chama wa uteuzi wa Wagombea nafasi za Ubunge, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na Udiwani, kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, utaanza rasmi May 01,2025 kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za maombi ya kuteuliwa kugombea nafasi hizo.

Taarifa iliyotolewa April 10,2025 na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Amos Makalla ilisema zoezi hilo litaanza May 01, 2025, saa 2:00 asubuhi na kumalizika May 15, 2025, saa 10:00 jioni na utaratibu wa kuchukua na kurejesha fomu za maombi kwa Wanachama wanaogombea nafasi ya Ubunge au Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa CCM wa Wilaya inayohusika.

Related Posts