Picha: Ali Kamwe awanoa Viongozi wa Klabu ya Pamba ya Mwanza

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga SC, Ally Kamwe akitoa semina kwa Viongozi wa Klabu ya Pamba Jiji kutoka Mwanza, jinsi mfumo wa Idara yetu ya Habari na Mawasiliano unavyofanya kazi.

Uongozi wa Pamba Jiji iliyopanda kushiriki Ligi Kuu ya NBC Msimu ujao, umefika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, Jangwani, Jijini Dar Es Salaam Leo, wakiwa na lengo la kujifunza kutoka Idara mbalimbali ndani ya Klabu ya Yanga zinavyofanya kazi.

Related Posts