PROFESA KITILA AFUNGUA WARSHA YA KUPITIA RASIMU YA RIPOTI YA UWEKEZAJI NCHINI YA MWAKA 2023

Na Mwandishi wetu Dodoma

Wataalamu na wadau wa sekta zinazohusika na shughuli za uwekezaji nchini wameshiriki katika warsha ya kupitia rasimu ya ripoti ya uwekezaji nchini ya mwaka 2023 na kutoa maoni yatakayosaidia Serikali kuwa na mfumo jumuishi wa ukusanyaji taarifa za uwekezaji nchini ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo.

Akifungua warsha hiyo, jijini Dodoma na Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, ametoa wito kwa wataalamu na wadau hao kuhakikisha wanatumia utaalamu na weledi ili kutoa mchango utakaoiwezesha Serikali kutoa taarifa za Uwekezaji zenye ukweli na ushahidi wa kisayansi.

Mhe. Prof. Mkumbo, amewaasa kujikita katika kutoa maoni ya kitaalamu ambayo pamoja na kupendekeza mfumo utakaotumika kutoa taarifa hizo, pia wahakikishe wanakubaliana kuhusu maudhui ya msingi yatakayotakiwa kuwekwa katika ripoti hiyo.

Aidha, amewataka kutoa mapendekezo kuhusu muda wa kutolewa ripoti hiyo inayotarajiwa kuwa na taarifa zote mahususi kuhusu uwekezaji, na kwamba iainishe taasisi itayokuwa na dhamana ya taarifa zinazohusu uwekezaji ili kurahisisha upatikani wa taarifa hizo.

Tangu kuanzishwa kwake Julai 2023, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji inatekeleza majukumu yake mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia masuala ya uwekezaji nchini.




Related Posts