Kuelekea maadhimisho ya wiki ya maziwa kitaifa ‘Kunywa Maziwa Salama kwa Afya Bora na Uchumi Endelevu’

Bodi ya Maziwa Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na wadau mbalimbali wa maziwa kila mwaka imekuwa ikiadhimisha Wiki ya Maziwa Kitaifa ambayo huwa inafanyika kuanzia mwishoni mwa mwezi Mei hadi mwanzoni mwa mwezi Juni na lengo ni kuwataka wadau mbalimbali nchini kuchangamkia fursa ya kufanya uwekezaji katika sekta ya maziwa kwani uzalishaji ni mdogo ukilinganisha na uhitaji.

Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa  yakiwa na dhana ya kuhamasisha unywaji wa Maziwa yaliyosindikwa na kuboresha soko la maziwa, dhana hiyo imekuwa ikibadilika na maadhimisho hayo kwa sasa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita yanalenga kuboresha wadau wote walioko kwenye mnyororo wa thamani (Value Chain) kuanzia mfugaji mpaka mlaji.

Kuelekea wiki maadhimisho haya malengo makuu ni Kuelimisha wananchi na umma matumizi ya maziwa kama chakula bora kwa watu wa rika zote na faida za maziwa katika kujenga afya ya binadamu.

Kuwaelimisha wadau kuongeza ubora wa bidhaa za maziwa zinazotengenezwa nchini ,kwaelimisha wadau umuhimu wa kujiunga na vyama vya Ushirika.

Akizungumza 21, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TVLA ambayo imelenga kuwajengea uwelewa kuhusu tasnia ya sekta ya maziwa, Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) Profesa George Msalya, amesema kuwa kwa sasa bado kuna uhitaji wa maziwa nchini jambo ambalo limepelekea Serikali kuanza kuagiza maziwa ya kutoka nje ya nchi.

‘Hali ya uzalishaji wa maziwa nchini ni lita bilioni 3.9, na sasa tunahitaji  lita bilioni 12 kwa mwaka’ hivyo bado mahitaji ya maziwa ni makubwa nchini.

“Licha ya kuwa na ng’ombe wengi nchini Tanzania na kuwa wa pili katika bara la Afrika,  lakini bado tunazalisha maziwa kidogo na hali hii kutokana wafugaji wengi hawatumii ng’ombe wa kisasa wa maziwa” amsema Profesa Msalya.

Maziwa, sote tunajua, yamejaa faida za kiafya na ni chanzo pekee cha lishe kwa watoto wachanga.

Lakini, swali ni, je, unakunywa maziwa safi zaidi? Je, lishe ya kioevu haijachafuliwa? Je, unahakikishaje kwamba ubora haujashuka? Jibu ni rahisi tumia maziwa yaliyosindikwa.

  

  

 

Related Posts