‘Kukutana na rais wa Kenya ilikua moja ya maono yangu’ Steve Harvey

Mtangazaji maarufu wa televisheni kutoka Marekani Steve Harvey  anasema kukutana na Rais William Ruto ni mojawapo ya mipango aliyokuwa nayo kwenye bodi yake ya maono.

Akizungumza kama mwenyeji wa Rais wa Kenya na ujumbe wake siku ya Jumanne, Harvey alisema itikio lake la kwanza alipoitwa kumwakilisha Tyler Perry ni jinsi ilivyokuwa bahati mbaya.

Aliendelea kusema kuwa ameonyesha bodi ya maono kwa Rais Ruto.

Nipo hapa kwa niaba ya  Tyler Perry, yuko nje ya mji na hakufanikiwa kufika. Alisema Steve,

  ”Rais wa Kenya anakuja mjini nikasema hiyo inashangaza kwa sababu yuko kwenye bodi yangu ya maono. Nilimuonyesha leo,” mtangazaji huyo wa TV alisema.

Harvey alibainisha kuwa tayari anafanya biashara na Rais wa Botswana, Eric Mokgweetsi na alikuwa akipanga kumshirikisha Rais Ruto.

Katika maelezo yake, Harvey alisisitiza kuwa Afrika ina uwezo mkubwa na hilo linahitajika ili kuziba pengo kati ya Afrika na ulimwengu wa nje.

Aliongeza kuwa bila ya Afrika, kusingekuwa na Waamerika wenye asili ya Afrika.

“Nilikuwa mtu wa kwanza kuleta kipindi cha Televisheni kutoka Marekani na kurekodi katika bara la Afrika baada ya kila mtu kuniambia haiwezekani.

Waliniambia kuwa haiwezekani,waliniambia hawana miundombinu ya kuiondoa nilienda huko na kuwathibitisha kuwa sio sahihi kwa sababu Afrika ina uwezo mkubwa zaidi.”

Related Posts